Breaking News

Maendeleo ya mradi wa Bwawa la Julius Nyerere yavuta hisia za wengi Saba Saba




Shirika la Umeme Tanzania,TANESCO  linashiriki  katika Maonesho ya kimataifa ya biashara ya sabasaba  kwa mwaka 2024.Maonesho haya yalianza  tarehe 28/6/2024 ambapo wananchi wengi wamevutiwa  kutembelea Banda la TANESCO ili kujionea maendeleo ya mkubwa wa kimkakati wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP)  ambalo limefikia asilimia 98.01 ya ujenzi wake kupitia miwani maalum ya uhalisia pepe (VR).

Akizungumza katika maonesho hayo Julai 1,2024 , Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano kwa Umma,Bi.Irene Gowelle amesema kuwa TANESCO imejipanga vyema katika ushiriki wake kwenye maonesho hayo ili kuwapa fursa wateja na  wananchi kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika sambamba na utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya umeme, Matumizi Bora ya  vifaa vya Umeme,Huduma za kidigitali ,elimu ya nishati safi ya kupikia na maboresho ya mita za LUKU yanayoendelea nchini.

Aidha amewasihi wananchi na wateja kutembelea Banda la TANESCO  na kusema kuwa pamoja na elimu inayotolewa lakini pia TANESCO imejipanga kuwazadiwa wateja wake vitu mbalimbali.

TANESCO inashiriki maonesho ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba hadi tarehe 13 Julai 2024

No comments