Breaking News

CHANGAMKIENI ASILIMIA 10 ZA MIKOPO YA HALMASHAURI .




- SOKO LA BWILINGU NI FURSA KWA KILA MTU  AELEZA MHE. MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze  Mhe.Ridhiwani Kikwete amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze kuwapeleka Maafisa Maendeleo kukutana na kina Mama, Vijana na Kina Baba ili kuwaelekeza namna yakuunda makundi yatakayowawezesha kukopa fedha kwaajili ya kunufaika na fursa mbalimbali za mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10  isiyo na riba ambayo imeanza kutolewa tena kuanzia tarehe 01.07.2024 baada ya Rais kuelekeza yafanyike maboresho ya utoaji mikopo hiyo ambayo inaokoa makundi maalum katika kujiinua kiuchumi.

Amesema "anataka vikundi vyenye utaratibu mzuri ambavyo vinatoa haki sawa kwa wanachama wote kunufaika na fedha hizo za mikopo na kwakuzingatia hakuna mtu mbabe, hakuna mtu mwizi, hakuna mtu anayetumia nafasi hiyo kujinufaisha mwenyewe kwakua moja ya jambo kubwa ambalo lilifanya utaratibu huo ukasimamishwa ni baadhi ya watu wanakuja katika jina la kikundi alafu fedha zinazoingizwa zinakwenda kwa mtu mmoja na yeye ananufaika pekeyake", alisema Mhe. Ridhiwani.

Ameyasema hayo kwenye mkutano na wananchi wa Chalinze mkoani Pwani ambapo ameongeza kuwa "maelekezo yameshatolewa na mimi kwangu ni maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha kwamba wananchi wa Chalinze hususani wafanyabiashara wanakua ni sehemu ya kundi la kwanza lakufaidika na fursa hiyo, aliendelea kusema Mhe. Ridhiwani

Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani amewaambia wananchi wa Chalinze kwa utaratibu waliojiwekea Baraza la Madiwani waliamua kutumia makusanyo ya ndani kwa kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa soko la Bwilingu na kununua baadhi ya majengo yaliyokuwepo katika eneo hilo ili kupata soko lenye ukubwa ambalo limewaweka wafanyabiashara wengi  kwenye eneo hilo, na litatumika na watu mbalimbali kutoka maeneo yanayozunguka eneo hilo na mikoa ya jirani kwaajili ya biashara zakujiingizia vipato.

Amesema "wananchi hawakukosea kuwachagua na kuwatuma viongozi wanaowatumikia kwakua wanatengeneza fursa ambalimbali zakibiashara bila ubaguzi kwa kuzingatia afya za wafanyabiashara na wateja wanaofika kupatiwa huduma katika eneo hilo, alisema Mhe.Ridhiwani.

Aidha amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha kila halmashauri kupata fedha hizo ambazo zinakwenda kuongeza vipato vya makundi maalum nakujikwamua kiuchumi.

No comments