Balozi Mbarouk kwa niaba ya Rais Dkt.Samia apokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Indonesia
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Mbarouk (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Indonesia, Mhe. Joko Widodo uliowasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe. Pahala Mansury. Ujumbe huo ulipokelewa tarehe 20 Julai 20, 2024 katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
No comments