Breaking News

ACT WAZALENDO ITAONDOA URASIMU NA KULIPA KODI KABLA YA KUANZA BIASHARA_ ADO SHAIBU

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndg. Ado Shaibu amesema chama hiko kitaweka mazingira mazuri ya kibiashara, kuondoa utitiri wa kodi kwa wakulima na shughuli zingine zinazochipukia katika uzalisha. Kauli hiyo ameisema ikiwa ni hatua ya kuongeza ajira na kuhakikisha kila Mtanzania ana shughuli ya kumpatia kipato.

"Mazingira ya sasa ya kiuzalishaji na biashara yana wakandamiza vijana walio wengi. ACT Wazalendo itaondoa mfumo wa kulipia kodi kabla ya kuanza biashara , itawapa uhuru wananchi na kuondoa urasimu katika kuanzisha biashara."

Ado Shaibu leo alikuwa Babati Mjini katika mwendelezo wa ziara ya chama hiko kuyafikia majimbo 2014 Tanzania Bara. Ametaja hatua ya kuhusianisha sekta ya uzalishaji wa ndani ili kutoa malighafi za kutekeleza miradi kwa ajili ya kutoa ajira kwa vijana.

No comments