Breaking News

Serikali yatoa kauli kuhusu hali ya huru wa kujieleza nchini, THRDC:Sheria ya makosa ya mtandao bado inabana.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Thobias Makoba akifungua kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari na kujieleza kwa niaba ya Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Naye lililoandaliwa na Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa kongamano la kujadili Sheria zinazosimamia vyombo vya habari na Uhuru wa kujieleza.


NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema itaendelea kuboresha mazingira ya kisera na kisheria ili kuimarisha zaidi Sekta ya Habari nchini.

Hayo yomebainishwa leo Juni 27, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Thobias Makoba akifungua kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari na kujieleza kwa niaba ya Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Naye.

Kwenye Kongamano hilo lililoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria wa Marekani (ABA) Makoba amesema chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kumeshuhudiwa mabadiliko makubwa katika tasnia hii kiasi cha kutoa Uhuru makubwa wa Vyombo vya Habari na kujieleza.

"Chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tumeona mageuzi makubwa kwenye Sekta ya Habari nchini. Serikali tunaamini kwenye mashirikiani na sio Mashindano. Kama Serikali tupo tayari kupokea maoni ya kuboresha kwa maslahi  ya tasnia hii," amesema Makoba.

Kwa upande wake Mratibu wa THRDC Wakili Onesmo Olengurumwa amesema lengo la kongamano hilo ni kujadili Sheria zinazosimamia vyombo vya habari na Uhuru wa kujieleza na kubainisha changamoto.

Kwamba kama THRDC wameshafanya uchambuzi wa kesi 30 na kubaini kuwa Sheria ya Makosa ya Mtandao inaongoza kwa kuvunja Haki ya kujieleza kwani imepeleka watu wengi mahakamani kwa tuhuma za makosa ya uchochezi na kusababisha taharuki.

Hivyo wanatakata kifungu cha 16 cha Sheria hiyo kifanyiwe mabadiliko kwani kimewapeleka watu wengi mahakamani na gerezani, kwamba ni lazima wajadili na Serikali kuona mabadiliko yanafanyika.

"Sheria ya Makosa ya Mtandao imevunja sana Haki ya kujieleza, watu wanakamatwa kamatwa hovyo bila kufuata utaratibu. Hivyo tumetoa mapendekezo yetu ya namba ya kuboresha Sheria zetu. Tunahitaji kuundwa kwa tuma ya pamoja ili kuzifanyia marekebisho ziendane na Wakati," amesisitiza Wakili Olengurumwa.

Kadhalika amesema kuwa tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mtaa baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, Sheria ya Uchaguzi inatakiwa kufanyiwa mabadiliko kwani inaminya Uhuru wa Vyombo vya Habari katika kuripoti taarifa za Uchaguzi.

"Tunapoelekea kwenye Uchaguzi ni Wakati wa kuwa na Uhuru wa kweli na wazi, kwani bila hivyo wananchi watashindwa kutoa maoni yao," ameeleza Wakili Olengurumwa.

Wakili Olengurumwa amebainisha kuwa vyombo vya habari vina wajibu wa kufikisha vilio vya wananchi kwa Serikali yao, hivyo ni lazima vilindwe.


No comments