Mbowe:Wananchi wa Karatu hawapaswi kuwa maskini
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema wananchi wa Karatu mkoani Arusha hawapaswi kuwa maskini kwakuwa mbali na mbuga zilizopo katika eneo hilo pia wanazalisha kitunguu bora ambacho kinauzwa nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika eneo la Mang’ola Karatu Mbowe amesemaenwo hilo lenye kilomita za mraba 3000 kati ya hizo kilomita 1000 ni ardhi ya kulima huku eneo lililobaki likizungukqa na hifadhi za misitu na mbuga za wanyama .
“Nyinyi mpo katika ya watu wenye bahati duniani , Mungu hakufanya makosa kuwapa hii baraka,hapa kwenye kata ya Eyasi kuna ziwa Eyasi,kuna ardhi bora yakuzalisha bitunguu,mbuga za wanyama ,mmepakana na Ngorongoro,Manyara,Tarangire zote hizo ni vitu vinavyoleta watalii,Mungu ana makusudi yake kuwaweka wananchi katika neema hii.
“Kuna watu wanakuja kama watalii wanalala kwenye hoteli ambazo chumba kimoja Dola za Marekani 5000 piga mahesabu kwa Sh 2000 kwa dola moja utajua wanalala shilingi ngapi kwa siku lakini mapato yote yanaenda serikali kuu hakuna mwana Karatu anafaidika ,ukienda halmashauri makato yote ya Ngorongoro,Tarangire yanaenda Dodoma wanaenda kugawana wenyewe wananchi hawana sauti na rasilimali zao ambazo zimewazunguka,”amesema Mbowe.
Akizungumzia kuhusu kilimo alisema katika eneo hilo kuna zao kuu la vitunguu lakini halina mfumo mzuri wa usimamizi hasa katika mapato kwa ajili yakusaidia wananchi mona kwa moja.
“Karatu awali halmashauri ilipokuwa inasimamiwa na Chadema ushuru wa gunia moja la kitunguu ulikuwa Sh 5,00 lakini sasa hivi halmashauri ipo chini CCM (Chama Cha Mapinduzi) ushuru umefika Sh 5,000 kwa gunia moja ,wananchi mnanyonywa hamuoni mmekuwa manamba kwenye zao la kitunguu na kuwafaidisha wengine .”alisema Mbowe.
Alisema Karatu mmebarikiwa kwa kilimo kwakuwa wanalima Kahawa ,Maharage ,Mbaazi,Ngani,Mahindi
Alisema eneo hilo pia lina madini ya gesso pamoja na mafuta ambayo yapi mbioni kugunduliwa pamoja na vyote hivyo bado wananchi wanakuwa maskini.
“Kuna madini adimi hapa ya gesi katika ziwa hilo la Eyasi,kuna mafuta msubiri tu siku yakikamilika mtaondolewa ,”alisema Mbowe.
Alisema ili wananchi waweze kufaidika na eneo lao wanapaswa wajiandikishe katika daftari la kupiga kura waweze kuuondoa uongozi wa CCM madarakani.
Awali Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara Tundu Lissu alisema serikali ya awamu ya tano imekuwa ikifanya mambo ya kudumaza maendeleo na uchumi ikiwemo kuuza bandari.
“Huyu mama ndani ya mwaka mmoja tayari kagawa bandari zetu kasema hatuwezi kuziendesha ,bandari ambazo zilisimamiwa na serikali za awamu zote ,kauza bandari zetu lakini za kwao hamna,serikali za awamu zote zimepita lakini hawakuwahi kugawa bandari,kaja aliingia Julius Nyerere,Ally Hassani Mwinyi,Benjamini Mkapa,Jakaya Kikwete,Magufuli (John Magufuli) wote waliweza kuendesha bandari,”alisema Lissu.
No comments