Breaking News

BRELA yatoa gawio kwa Serikali kwa taasisi za umma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan jana tarehe 11 Juni, 2024, amepokea gawio la kiasi cha TZS  Bilioni Kumi na Nane Mia Tisa Sabini na Tatu, Millioni Mia Nane Hamsini na Tatu Elfu, Mia Tano Kumi na Nne na Senti Ishirini na Saba tu (18,973,853,514.27) kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ikiwa ni utekelezaji wa utoaji gawio  kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370. Hafla hiyo imehudhuriwa na Dkt Fred Msemwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Waziri kwa BRELA na Bw Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA.





No comments