WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA NBAA KWENYE MAONESHO YA ELIMU MKOANI TANGA
BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imejipanga kuhakikisha inaendelea kutoa Elimu kwa wananchi katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, ujuzi na ubunifu mwaka 2024 yenye kauli mbiu isemayo "Elimu, ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani" yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Ameyasema hayo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Magreth Kageya kuwa wanatoa huduma zote ikiwemo kutoa maelekezo ya jinsi ya kujisajili kwa ajili ya kufanya Mitihani, maelezo juu ya ulipaji wa ada mbalimbali na pia ametoa wito kwa wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya NBAA.
Pia amesema lengo kuu ni kutoa Elimu na uelewa juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NBAA
Aidha, amesema baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha maonesho ya elimu ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya Kihasibu na Kikaguzi.
Hivyo, amesisitiza kuwa Bodi hiyo kwa sasa inatumia mifumo ya kidijitari kutoa huduma zake kwa kupitia tovuti yao.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/E7vn6kZ
No comments