Breaking News

NMB YATOA FURSA KWA VIJANA WENYE BUNIFU MBALIMBALI HAPA NCHINI

MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka  Ladislaus akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda ambapo alisema kwamba benki hiyo inatambua umuhimu wa ubunifu katika maendeleo ya nchi.
MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka  Ladislaus kulia akifurahia Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda kushoto wakati alipotembelea banda lao wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo 



Na Oscar Assenga, Tanga.

BENKI ya NMB imeshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly huku wakitoa fursa kwa vijana wenye bunifu mbalimbali kwenda kufanya majaribio kwenye benki hiyo.

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda ambapo alisema kwamba benki hiyo inatambua umuhimu wa ubunifu katika maendeleo ya nchi.

Alisema kwamba wao kama benki pamoja na ufadhili wanatoa Jukwaa Maalumu (Platfom) kuwakaribisha vijana kufanya ubunifu, maendeleo ya kibunifu na miradi hiyo wamekuwa wakiifadhili.

“Kwa niaba ya Benki ya NMB niwaambie kwamba tunatambua umuhimu wa ubunifu na ndio maana tumeungana nanyi katika wiki hii kwa kuwa elimu ndio inachochea ubunifu sisi kama Benki pamoja na mfadhili tunatoa jukwaa maalumu kuwakaribishasha vijana kuja kufanya ubunifu kufanya maendeleo ya kibunifu na miradi hiyo tunaifadhili”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba na inasaidia kuleta chachu ya kuendelela kuleta mendeleo ya ubunifu Tanzania hivyo wataendelea kuwaunga mkono kuhakikisha maendeleo ya sekta hiyo yanapiga hatua kubwa.

“Mh Waziri niwakaribiha vijana wenye bunifu mbalimbali waje kufanya majaribio yao kwenye benki ya NMB tuna platfomu NMB Sign Box nzuri inatoa nafasi nzuri ya bunifu tupo tayari kushirikiana nao kama Wizara kuhakikisha ubunifu unaleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi hapa nchini”Alisema

Awali akizungumza wakati akifungua maadhimisho hayo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda Serikali imesema ipo katika mchakato wa kujenga shule 100 za mafunzo ya Amali nyanja ya ufundi nchi nzima ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kuweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi watakaopata kupitia vyuo hivyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Pastrobas Katambi amesema dunia ya sasa ina mabadikiko makubwa hasa kwenye masuala ya sayansi na teknolojia ujuzi na ubunifu hivyo ni wakati wa vijana wa kitanzania kwenda sambamba na mabadiliko hayo.

Awali Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Profesa Carolyne Nombo alisema wanafunzi 27 walishinda shindano la ujuzi na ubunifu ngazi ya vyuo ambao watafanyiwa mchakato na kupatikana wanafunzi 3 wa fani tofauti ambao watakwenda kushiriki mashindano ya kikanda na kimataifa mapema mwaka 2025.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko amesema bunifu zinazoibuliwa katika maeneo mbalimbali nchini zitengenezwe katika uhalisia ili kuleta tija kwa jamii na kiuchumi.

Mwenyeji wa maadhimisho hayo ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani alisema mkoa wa Tanga umepokea trilioni 2 na milioni 600 kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu ambapo shule mpya 27 zimejengwa pamoja na vyuo vya kati ambavyo vipo katika hatua mbalimbali.



from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/Wcu2NX9

No comments