KAMOGA: MIFUMO IMARA IMESAIDIA KUONGEZA KODI
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipakodi na Mawasiliano kwa umma, Hudson Kamoga amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mifumo imara waliyoianzisha imesaidia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza katika semina ya waandishi wa habari za mitandao ya kijamii Dar es Salaam leo Mei 29, 2024 Kamoga amesema kwa miaka mitatu iliyopita ya Rais Samia Suluhu Hassan, TRA imeongeza mapato kutoka trilioni 18 mwaka 2021/2022 hadi trilioni 24 mwaka 2022/2023.
Amesema mafanikio hayo yamechagizwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Watanzania kutambua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari kupitia utoaji elimu unaofanywa na TRA.
Kamoga ameongeza kuwa TRA imeimarisha mifumo yake ya ukusanyaji kodi ambapo mambo mengi kwa sasa yanafanyika kupitia mifumo ya kidigitali badala ya ukusanyaji wake wa kawaida ambayo ilikuwa inawachukua muda mrefu kukusanya mapato.
“Katika mazingira ya namna hii mambo mengi yamerahisishwa na watu wamekuwa na hiari ya kulipa kodi na ukwepaji wa mapato umepungua kwa kiasi kikubwa sana na tunatarajia ifikapo mwezi wa 8 mwaka kesho kutakuwa na mfumo maalum ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa ukwepaji wa kodi,” amesema Kamoga.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mifumo imara waliyoianzisha imesaidia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza katika semina ya waandishi wa habari za mitandao ya kijamii Dar es Salaam leo Mei 29, 2024, Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipakodi na Mawasiliano kwa umma, Hudson Kamoga amesema kwa miaka mitatu iliyopita ya Rais Samia Suluhu Hassan, TRA imeongeza mapato kutoka trilioni 18 mwaka 2021/2022 hadi trilioni 24 mwaka 2022/2023.
Amesema mafanikio hayo yamechagizwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Watanzania kutambua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari kupitia utoaji elimu unaofanywa na TRA.
Kamoga ameongeza kuwa TRA imeimarisha mifumo yake ya ukusanyaji kodi ambapo mambo mengi kwa sasa yanafanyika kupitia mifumo ya kidigitali badala ya ukusanyaji wake wa kawaida ambayo ilikuwa inawachukua muda mrefu kukusanya mapato.
“Katika mazingira ya namna hii mambo mengi yamerahisishwa na watu wamekuwa na hiari ya kulipa kodi na ukwepaji wa mapato umepungua kwa kiasi kikubwa sana na tunatarajia ifikapo mwezi wa 8 mwaka kesho kutakuwa na mfumo maalum ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa ukwepaji wa kodi,” amesema Kamoga.
Chanzo: Sautikubwa
No comments