TRA YAPONGEZA NGUVU YA MAJUKWAA YA KIDIJITALI KATIKA KUHAHARISHA UMMA
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi na mawasiliano wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Hudson Kamoga
Mwenyekiti Jukwaa la Wanahabari wa mtandaoni (JUMIKITA) Shabani Matwebe
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wamekutana na waandishi wa habari wa mtandaoni katika Semina waliyoiandaa kwa kushirikiana na Jukwaa la Wanahabari wa mtandaoni (JUMIKITA) leo Mei 29 ,2024, Imefanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere I (JNICC) Jijini Dar es salaam
" TRA ni Taasisi ya kwanza kugundua nguvu ya Digital Platform, Nyie mnajua ni jinsi gani mnapata tabu kupata taarifa ikitokea mtu amewatambua ni lazima tumpongeze, Digitali Platform haikwepeki, Mkurugenzi nikupongeze "
Mwenyekiti Jukwaa la Wanahabari wa mtandaoni (JUMIKITA) Shabani Matwebe
Lakini pia, wawakilishi kutoka mamlaka ya TRA walitoa neno huku wakikumbusha wajibu wa kila mwananchi kwenye suala la ulipaji kodi kupitia kudai risiti ,"Mwamko wa Wananchi kudai risiti za EFD ni mdogo, waandishi wa Habari wa mitandao ya kijamii mnalojukumu la kutumia taaluma na weledi wenu kuuelimisha uuma juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kudai risiti wanaponunua kitu chochote.
"unapoacha kudai risiti unakuwa umemsaidia muuzaji kupunguza kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa"Hayo yamesemwa Mei 29,2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipakodi na mawasiliano wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Hudson Kamoga wakati wa semina ya masuala ya kodi kwa waandishi wa habari mitandaoni yaliyotolewa na TRA Jiini Dar es salaam.
No comments