Breaking News

WAZIRI JAFO AKUTAJNA NA WATUMISHI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amehimiza Umoja, Amani, Upendo na Mshikamano kwa Watumishi wa Ofisi hiyo ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo na kuharakisha kasi ya kuimarika kwa Muungano na hifadhi endelevu ya Mazingira.

Dkt. Jafo ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika hafla ya ukaribisho wa Katibu Mkuu, Mhandisi Cyprian Luhemeja aliyewasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma kuanza kutekeleza majukumu yake ya kazi  Aprili 8, 2024.

Waziri Jafo amesema rasilimaliwatu imara katika wizara, idara na taasisi ya umma inajengwa na misingi ya umoja, amani, upendo na mshikamano na iwapo misingi hiyo itazingatiwa Ofisi husika itapiga hatua kuwa ya maendeleo huku akitolea mfano Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo katika kipindi cha miaka mitatu imepata mafanikio makuwa katika kuimarisha Muungano na hifadhi endelevu ya Mazingira.

Akitolea mfano amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ofisi ya Makamu wa Rais imepata mafanikio makuwa katika masuala ya Muungano na Mazingira, ambapo jumla ya Hoja 15 za Muungano zimepatiwa ufumbuzi na katika eneo la Mazingira Ofisi hiyo kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuongezewa fedha za kutekeleza miradi malimali.  

“Mwezi machi mwaka huu nimetimiza miaka mitatu katika Ofisi hii na kwa pamoja tumeleta mafanikio makubwa na yanayoendelea kuleta sifa na heshima kwa kiongozi wetu mkuu Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory Mpango amaye ana majukumu ya kikatia ya kuwa mshauri wa kwanza wa mhe. Rais lakini pia kusimamia masuala ya Muungano na hifadhi ya Mazingira,” amesema Dkt. Jafo.

Aidha, amemtaka Mhandisi Luhemeja kushirikiana kwa karibu na watendaji na watumishi wa Ofisi hiyo kwani wengi wao wana uzoefu, weledi, nidhamu na maarifa ya hali ya juu katika utendaji kazi na hivyo kuweza kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake.

Akifafanua zaidi waziri jafo amewataka watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa idii, nidhamu na maarifa kwani kwa upande wao kama viongozi wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaendelea kuimarisha mazingira ora ya kazi pamoja na kuoresha maslahi malimali ya watumishi.

Dkt. Jafo pia amewataka wakuu wa idara na vitengo pamoja watendaji na watumishi ndani ya ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa pamoja, kuimarisha ushirikiano na mahusiano ili kuhakikisha mafanikio makuwa zaidi yanaendelea kupatikana na hivyo kuendelea kuleta sifa kwa viongozi wa ofisi hiyo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Jafo pia amemwelekeza mhandisi luhemeja kusimamia kwa kariu ujenzi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika mji wa serikali, mtuma jijini Dodoma na kuhakikisha kuwa mkandarasi husika anakamilisha kazi hiyo kwa wakati na muda uliopangwa.

“Siridhishwi na kasi ya mkandarasi anayehusika katika ujenzi wa jengo la ofisi yetu, hivyo nakuagiza kwa kufuatilia kwa kariu ujenzi wa jengo hilo ili kuweza kukamilika na kuanza kutumika” amesema Dkt. Jafo. 

Kwa upande wake, mhandisi Luhemeja alimshukuru waziri jafo kwa maelekezo aliyotoa kwa watendaji na watumishi wa ofisi hiyo na hivyo kuahidi kuyafanyia kazi kwani dhamira ya serikali ni kuhakikisha watumishi wa umma wanaendelea kufanya kazi katika mazingira ora na wezeshi.

“Nakushuru mhe. Waziri kwa maelekezo uliyotupatia sisi watendaji na watumishi sote tunaahidi kuyafanyia kazi ili kuhakikisha tunasukuma mrele gurudumu la maendeleo ya ofisi hii amayo ina jukumu kuwa katika kuimarisha Muungano na hifadhi endelevu ya Mazingira” amesema mhandisi luhemeja.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi na Watendaji mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwemo Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware.

Itakumbukwa kuwa kabla ya kuhamia Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Luhemeja alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).

    

No comments