Breaking News

VICTORIA FOUNDATION YAKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA SHULE 25 MKOANI GEITA

  
Taasisi ya Victoria Foundation kwa kushirikiana na Orica Tanzania inatekeleza mradi wa hatua kwa hatua uitwao Binti Ng'ara, kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa kike kupata taulo za kike za kumuwezesha Binti aweze kwenda shule wakati wote hasa wa siku zake za Hedhi. 
 
Katika hafla ya Ugawaji wa Taulo hizo uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Nyankumbu Tarehe 18 April, Mgeni Rasmi alikua ni Afisa Elimu Sekondari Cassian Luoga akimuwakilisha katibu Tawala Mkoa wa Geita. Hafla hiyo ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Orica Tanzania, Asha Mambo, Kaimu Mkurugenzi  Taasisi ya  Victoria Foundation Steven T. Mruma, Mkurugenzi na Mzalishaji wa Taulo za Kike za Palesa Sherie De Wity kutoka Nchini Afrika kusini, Maafisa Elimu wa ngazi mbalimbali , Muwakilishi wa Dawati la Jinsia Kutoka Jeshi la Polisi Afande  Christina Katana pamoja na Walimu na Wanafunzi kutoka shule sita za Wilaya Ya Geita Mji. 

Taulo hizo za kike zitawanufaisha Jumla ya  wasichana 2500 kutoka Shule 25 za mkoa wa Geita kutoka katika Wilaya zote Sita ambapo box moja la taulo za kike linaweza kutumiwa na Mwanafunzi kwa muda wa miaka mitano kwakua Taulo hizo zinaweza kufuliwa na kutumika tena (Re usable), Zilizotengenezwa na kampuni ya Palesa Pads kutoka nchini Africa ya Kusini.

Akizungumza katika hafla hiyo ya ugawaji Mgeni Rasmi Cassian Luoga aliwashukuru Orica Tanzania kwa kufadhili mradi wa Binti Ng'ara chini ya Taasisi ya Victoria Foundation na kuomba wadau wengine wajitokeze kwa wingi ili kusaidia kutatua kabisa tatizo la wasichana kukosa vipindi vya Darasani kutokana na kukosa taulo za kike hasa wakati wakiwa katika hedhi. 

Nae Mkurugenzi Wa Orica Tanzania Asha Mambo aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na Taasisi zisizo za serikali kukabaliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili mabinti. 

Akitoa shukrani  kwa niaba ya Mkurugunzi  wa Victoria, 'Vicky Kamata',Maneja wa Miradi wa Taasisi hiyo Ndugu Steven T. Mruma aliwashukuru Orica Tanzania kwa Ufadhili wa Mradi,  na Uongozi wa Mkoa wa Geita kwa ushirikiano mkubwa walioutoa wakati wote  wa utekelezaji wa Mradi huo.











No comments