TUMELETEWA WATAALAMU ILI TUPATE PARACHICHI KWA UHAKIKA" - MKULIMA MBEYA
Mkulima Silvester Thomas Kayombo kutoka Mbeya anayejihusisha na Kilimo cha parachichi aishukuru wizara ya Kilimo kwa kulifanya zao la parachichi kuwa zao la kimkakati na kuwapelekea wataalamu (maafisa ugani) wanaowasaidia kupata tunda hilo kwa uhakika.
Kayombo ameeleza namna serikali kupitia Wizara ya Kilimo inavyowasaidia kufanya kilimo cha kisasa kwa kuwapelekea wataalamu pamoja na serikali kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa unaowawezesha wakulima kuuza/kusafirisha mazao yao nje ya nchi.
Aidha Mkulima huyo ameeleza kuwa serikali imewapelekea mbegu bora na za muda mfupi ambapo ndani ya miaka miwili na nusu hadi mitatu mkulima anaanza kuvuna parachichi.
"Parachichi limenisaidia, nimejenga, nafuga na kusomesha kwa kilimo cha parachichi, kweli tukifuata maelekezo ya wataalamu tunapata mapato mazuri" - Aliongoza Silvester Thomas Kayombo
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/wekdh71
No comments