TUME YA ATOMIC YAZIDI KUPAA KITEKNOLOJIA
Na Tunu Bashemela
SERIKALI ya Awamu ya Sita kupitia Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (Tanzania Atomic Energy Commission-TAEC) imeendelea na juhudi za kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyukilia nchini.
Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Prof.Lazaro Busagala katika kikao kazi na waandishi wa akieleza mafanikio ya Tume hiyo.
"TAEC imefanya juhudi kubwa kuhakikisha wananchi wanaelewa fursa zilizopo katika matumizi salama ya sayansi ya nyuklia kwa ajili ya kujilitea maendeleo. Ambapo TAEC imeongeza program za kujitangaza kutoka 12 hadi 60 kwenye TV, Redio, magazeti, mitandao ya kijamii na kushiriki katika maonesho mbalimbali," alisema Prof. Busagala.
Kwamba katika kuboresha tafiti za teknolojia ya nyukilia, Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kuongeza tengeo la bajeti ya utafiti kwa TAEC hadi kufikia Tsh 450M katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Alisema Juhudi hizi zimefanyika ili kupata fursa zaidi za sayansi na teknolojia ya nyukilia na pia kuwalinda wananchi na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi ambapo katika miaka mitatu machapisho 25 yakitafiti yamepatikana katika juhudi hizi.
Prof. Busagala akizungumzia kuhusu ununuzi wa vifaa vya sayansi na teknolojia ya nyuklia, alisema Vifaa vya kisayansi ni nguzo muhimu katika kudhibiti athari za mionzi, tafiti, usimamizi na uendelezaji wa Teknolojia ya Nyuklia.
"Serikali ya Awamu ya Sita, inaendelea kuweka
bajeti na kununua vifaa. Vifaa vya jumla ya TSh. 2.9 Billion vinaendelea
kununuliwa," alieleza Prof. Busagala.
Alibainisha mafanikio mengine kuwa ni kuongeza
usimamizi wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya nyuklia, kwamba Serikali ya
Awamu ya Sita imeendelea na juhudi za kusimamia udhibiti wa matumizi salama ya
mionzi ili kuepuka madhara yake.
Kwamba hadi mwaka 2022/2023 jumla kaguzi 971 kwa mwaka zilifanyika ukilinganisha na kaguzi 244 kwa mwaka 2016/2017, hili ni ongezeko la asilimia 298 na alieleza kuwa kaguzi hizi ni nyingi kuliko viwango vya kimataifa vinavyotakiwa.
Katika hatua nyingine Prof. Busagala alieleza kywa
TAEC imefanikiwa kuongeza makusanyo ya maduhuli ya Serikali kutoka shilingi
bilioni 8.7 mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia shilingi bilioni 10.9 mwaka
wa fedha 2022/2023.
No comments