GILITU AZINDUA MASHINDANO YA UMISETA KANDA YA MWASELE
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari Lubaga Gilitu Makula akipongezana na mwalimu mkuu wa Shule ya sekondari Lubaga Hamisa Boniphace
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari Lubaga Gilitu Makula akizungumza baada ya kuzindua mashindano ya umiseta
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Lubaga manispaa ya Shinyanga Gilitu Makula amezindua mashindano ya umiseta kanda ya Mwasele yenye shule za sekondari nne ambazo ni
Lubaga, Mwasele, Mwangulumbi na Hope Extended katika shule ya Sekondari Lubaga.
Akizindua mashindano hayo leo tarehe 16.04.2024 Makula yaliyofanyika katika shule ya Lubaga manispaa ya Shinyanga amewasihi walimu kuadhimisha na kuendeleza michezo maana michezo ni afya, na ni ajira na michezo hudumisha mahusiano.
Akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule hizo Makula ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi amewashauri kuendeleza michezo, na ameahidi kutoa zawadi kwa washindi wote watakao vuka hatua hii ya kanda na kwamba siku ya mwisho ya mashindano atatoa chakula kwa walimu na wanafunzi wote kwa shule zote nne.
Naye Mkuu wa Shule ya Lubaga Hamisa Boniphace kwa niaba ya wakuu wa shule wa kanda ya Mwasele alimshukuru Makula kwa kuwa na moyo wa kujitoa kwa jamii hasa katika sekta ya elimu na michezo
"Ndugu mgeni rasmi na mwenyekiti wetu Bodi ya shule ya Lubaga, tunakupongeza kwa dhati kwa namna ambayo umekuwa ukijitoa, Ikimbukwe na wewe mwenyewe ulituwezesha magori ya mpira wa miguu na wavu, magori na wavu wa volleyball pamoja na magoli ya mchezo wa pete," amesema Hamisa.
"Pia tunakushukuru kwa kutupatia jezi za kutosha na mipira mitano, na hii imekuwa ndiyo sababu ya shule yetu ya Lubaga kuchaguliwa kuwa kituo cha michezo katika kanda yetu hii ya Mwasele, hivyo Mwenyekiti tunakushukuru sana tena sana kwa kujitoa kwako",ameongeza
Hamisa pia amrwaasa wanafunzi kuwa na nidhamu wakati wote wakiwa kwenye michezo hapo Lubaga na hata baada ya Lubaga".
Naye diwani wa kata ya Lubaga Reubeni Dotto amempongeza Makula kwa namna alivyo karibu na jamii yake kwa kuendelea kutoa misaada mbalimbali katika shule hiyo na katika jamii.
Afisa elimu kata ya Lubaga Mwalimu Godfrey Mutungi amewaasa wanafunzi kuwa na nidhamu na kujituma katika michezo, ambapo michezo ya umiseta imezinduliwa wiki hii katika ngazi za kanda.shule ya Lubaga.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/RLyudFe
No comments