OSHA KUENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WANAOKIUKA KANUNI MAHALA PA KAZI
Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Katika ukumbi wa habari Maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu yake.
****
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umeyatoza faini maeneo ya kazi ambayo hayakuzingatia sheria na kanuni ikiwa ni pamoja na kuyachukulia hatua mbali mbali za kisheria zikiwemo kupewa hati ya maboresho ambapo maeneo ya kazi 1,588 yalipewa hati hizo huku 105 yalitozwa faini.
Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda amesema hayo leo March 4,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita na kwamba hatua hiyo imeboresha usalama na afya kwa lengo la kuzuia ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi.
Amesema, katika kuimarika kwa shughuli za usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi OSHA imefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 11,953 ongezeko hilo ni sawa asimilia 276.
"Idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia Kaguzi 322,241 sawa na asilimia 132,kumekuwa na ongezeko la asilimia 175 ya wafanyakazi waliopata mafunzo ya Usalama na afya mahali pa kazi kutoka wafanyakazi 32,670 hadi kufikia wafanyakazi 43,318;
Mafunzo hayo yanajumuisha mafunzo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na uundwaji wa kamati za usalama na afya ,mafunzo ya kufanya kazi za mazingira ya juu mafunzo ya huduma ya kwanza, mafunzo ya usalama na afya katika sekta ya mafuta na gesi na katika sekta ya ujenzi na majenzi na mafunzo ya usalama wa mitambo," amesema.
Mkurugenzi huyo pia amesema OSHA imeongeza kasi upimaji afya za wafanyakazi kwa asilimia 320 kutoka wafanyakazi 363,820 hadi kufikia milioni 1.1 na kwamba ongozeko hilo ni tafsiri kwamba hali ya usalama na afya katika maeneo ya kazi inazidi kuimarika.
"Kuhusu kupungua kwa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi Khadija OSHA ilichunguza ajali mbali mbali zinazotokea katika sehemu za kazi kwa lengo la kubaini vyanzo vya ajali hizo ili kushauri namna bora ya kuzuia ajali kutokea tena;
Vile vile kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa ajali zilizoripotiwa zilipungua kwa asilia 13.2 kutoka ajali 2,138 kupungua hadi kufika 1,855,"amefafanua.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/b37RGiS
No comments