Breaking News

BUNGE LA AFRIKA LAHAMASISHA MATUMIZI YA DAWA ZA ASILI

Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika iliyoshirikisha Wabunge wa Bunge la Afrika na Wadau mbalimbali wa afya katika Ukumbi wa Bunge la Afrika, Mdrand Afrika Kusini.

Dkt. Gayo amesema kuna uhitaji mkubwa kukuza dawa za asili ili kuwezesha kuunganishwa kwake katika mifumo ya afya barani Afrika.

"Tunataka kukuza tiba asilia katika nchi zetu za Afrika ili kuchangia katika kuboresha huduma ya afya ya watu wetu lakini pia kuhakikisha nafasi ya dawa za asili katika mifumo ya afya inatambuliwa. Tunataka pia kuhakikisha dawa za asili zinaboreshwa kisasa lakini pia Sheria zinaimarishwa ili kudhibiti utafiti katika dawa za asili",amesema Dkt. Gayo.
Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Pili wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) Mhe. Dkt. Ashebiri Gayo kutoka Ethiopia akizungumza leo Jumatano Machi 15,2023 wakati anafungua
Warsha ya Pamoja juu ya nafasi ya dawa za asili (Traditional medicine) katika mifumo ya afya ya Afrika

from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/MSaHvAp

No comments